Moto unaosababishwa na short ya umeme ni hatari sana kwa sababu:
a. Huenea kwa kasi
b. Huambatana na mshtuko wa umeme
c. Hauzimiki kwa maji
d. Husababisha vifo na uharibifu mkubwa wa mali
Ndiyo maana ni muhimu kuchukua hatua sahihi haraka na kwa usalama.
1️⃣ KATA UMEME HARAKA
Hatua ya kwanza kabisa ni:
a. Zima main switch, MCB, au fuse box
b. Kama huwezi kufika salama, usijaribu kugusa waya au vifaa vya umeme
👉 Kukata umeme kunazuia:
a. Moto kuendelea kuongezeka
b. Hatari ya kupigwa na mshtuko wa umeme
2️⃣ TOA TAARIFA YA DHARURA
Mara baada ya kuona hali ni hatari:
c. Pigia Zimamoto – 112
b. Waambie kuna moto wa umeme na eneo husika
📞 Pia toa taarifa TANESCO kwa kupiga namba 180
a. TANESCO wanaweza kusaidia kukata umeme wa nje au kutoa msaada wa kiufundi
b. Hii ni muhimu hasa kwenye ofisi, viwanda au maeneo yenye transfoma karibu
3️⃣ ZIMA MOTO KWA KIZIMA MOTO SAHIHI
Ikiwa moto bado ni mdogo na upo salama:
a. Tumia kizima moto cha umeme (CO₂ au Dry Powder)
b. Lenga chini ya moto, sio juu ya moto
❌ USITUMIE MAJI
a. Maji huongeza hatari ya mshtuko wa umeme
b. Moto wa umeme unaweza kuongezeka zaidi
4️⃣ TOKA HARAKA KAMA HAKO SALAMA
Kama moto unaongezeka:
a. Toka mara moja kupitia njia ya dharura (EXIT)
b. Usirudi kuchukua mali zako
c. Jifunike pua na mdomo kwa kitambaa kama kuna moshi
👉 Maisha ni muhimu kuliko mali
5️⃣ WATOE WENGINE NA SAIDIA WENYE MAHITAJI
a. Hakikisha watoto, wazee na watu wenye ulemavu wanatoka salama
b. Usisukumane
c. Tumia ngazi, usitumie lifti
6️⃣ KAA MBALI NA ENEO HATARI
Baada ya kutoka:
a. Kaa mbali na jengo
b. Usikaribie waya zilizoanguka au vifaa vya umeme
c. Subiri maelekezo ya zimamoto au TANESCO
7️⃣ BAADA YA MOTO KUDHIBITIWA
a. Usirudishe umeme bila fundi mtaalamu
b. Fanya ukaguzi wa mfumo mzima wa umeme
c. Badilisha nyaya zilizochomeka au vifaa vilivyoharibika
⚠️ USHAURI WA JUMLA
✔ Tumia fundi umeme mwenye leseni
✔ Usipakie umeme kupita uwezo wa mfumo
✔ Tumia vifaa bora (MCB, RCD, nyaya halali)
✔ Weka kizima moto karibu na fuse box
🌍 Kwa Elimu Zaidi
Tovuti: 👉 https://tanzaniawiring.co.tz
Huduma za umeme salama & ushauri wa kitaalamu
All News
Back Home
Maoni