1️⃣ WAYA WA NDANI YA TUBE / NYUMBA (SINGLE CORE – PVC)
Hutumika kwenye mfumo wa kawaida wa majengo (residential wiring).
Saizi na matumizi yake:
a) 1.5mm² (10 Amps) – Kwa taa (lighting)
b) 2.5mm² (20 Amps) – Kwa soketi (plug points)
c) 4mm² (25–32 Amps) – Kwa vifaa vyenye matumizi ya juu kama jiko la umeme
d) 6mm² – 10mm² (35–45 Amps) – Kwa main supply au mashine zenye mzigo mkubwa
Rangi za kawaida:
a) Nyekundu / Kahawia – Live (Phase)
b) Nyeusi / Bluu – Neutral
c) Kijani na Njano – Earth
2️⃣ WAYA WA EARTHING (GROUND WIRE)
a) Waya huu hulinda watu na vifaa dhidi ya mshtuko wa umeme.
b) Rangi yake ni Kijani chenye mistari ya Njano
Kwa kawaida hutumia:
a) 2.5mm² (kwa mfumo wa kawaida wa nyumba)
b) 4mm² au zaidi (kwa mzigo mkubwa au viwandani)
c) Earthing ni muhimu sana kwa usalama wa mfumo mzima wa umeme.
3️⃣ WAYA WA VIFAA VYENYE MATUMIZI MAKUBWA
Hutumika kwa mashine, pampu, jiko la umeme, AC n.k.
a) 2.5mm² (hadi 20–25A)
b) 4mm² (hadi 32A)
c) 6mm² (hadi 40A)
d) 10mm² (hadi 50–55A)
⚠ Chagua waya kulingana na mzigo wa kifaa (Amps), si kwa kukisia.
4️⃣ AINA NYINGINE ZA WAYA
a) Flexible cable – Kwa vifaa vinavyohama kama pasi, friji, pampu
b) Armoured cable – Kwa matumizi ya nje au chini ya ardhi
c) Conduit wiring (PVC au chuma) – Kulinda waya ndani ya ukuta
MAMBO YA MUHIMU KUZINGATIA
✔ Chagua saizi ya waya kulingana na mzigo wa umeme (Amps)
✔ Hakikisha waya zina alama za ubora (mfano TBS)
✔ Epuka kutumia waya ndogo kwa mzigo mkubwa
✔ Tumia fundi umeme mwenye leseni
Tovuti:
🌐 tanzaniawiring.co.tz
All News
Back Home
Maoni