Changamoto zinazosababisha vifaa vitumiavyo umeme ndani ya nyumba kuungua

Eng mwakinyo Juma | January 29, 2026
News Image
Zifuatazo ni baadhi ya changamoto zinazotokea na kusababisha kuunguza vifaa vitumiavyo umeme ndani ya nyumba yako:

1. EARTHING SYSTEM KUWA DHAIFU AU KUCHOKA.
Earthing system ni moja ya system muhimu katika miundombinu ya umeme,hufanya kazi Kama kusawazisha matumizi ya umeme,lakini pia hutumika kama njia ya ulinzi wa vyombo vya umeme Kama umeme ukizidi.kwa kawaida earthing system inatakiwa iwe na ukinzani(resistance) mdogo ili umeme unaozidi uweze kwenda ardhini na Kupotea huko usilete madhara kwa mtumiaji,moja ya kitu chenye ukinzani mdogo kwa umeme ni ardhi,hivyo earthing system hufungwa ardhini.System hii ikianza kuchoka husababisha ukinzani kuwa mkubwa na kupelekea pia matumizi ya umeme kuongezeka,huchangiwa kwa kiasi kikubwa na earthing system kuchoka au kufungwa chini ya kiwango.Earthing system ikiwa dhaifu huwa hatari zaidi hasa kipindi cha radi,nyumba au kiwanda huweza kupigwa na radi Kirahisi na ikaleta madhara.

2. LOOSE CONNECTION KWENYE MIUNDOMBINU YA UMEME.
Kwenye nyumba au kiwanda,kunakuwa na connections au junctions mbalimbali za nyaya za umeme,hivyo zikifungwa na kukaa muda mrefu au zikifungwa chini ya kiwango husababisha loose au kulegea .loose connection ina madhara makubwa sana maana huweza kusababisha nyumba kuungua kutokana na nishati ya umeme(voltage na current),na pia huweza kuunguza baadhi ya vyombo vinanyotumia umeme.

3. MIUNDOMBINU YA UMEME KUCHOKA
Mfano mzuri uliopo na unaofahamika na wengi ni circuit breaker au switches vikianza kuchoka hushindwa kujizima pale inapotokea umeme umezidi.

Hivyo Ndugu Mteja hakikisha unazingatia mambo yafuatayo:

1. Hakikisha mifumo yako ya umeme inasukwa na mtu aliyebobea na anatambulika na mamlaka husika.
2. ⁠Hakikisha unafanya ukaguzi au matengenezo ya Wiring System kila baada ya miaka 5 kwa nyumba za kuishi na miaka 3 kwa wateja wa viwanda.
All News Back Home

Maoni